Swahili
Kilimo hai ni nini?
Kilimo hai huwiana na kuendeleza mazingira bali sio kufanya kinyume. Huu ni mfumo wa kutumia viungo vilivyo hai na vinavyopatikana kwa urahisi pasipo kudhuru mazingira au binadamu. Kwa kifupi twaweza kueleza matumizi ya viungo hivi kama ifuatavyo:
Kuimarisha na kujenga rutuba ya mchanga:
• Mabaki ya mimea kwa pamoja na samadi au mkojo wa mifugo.
• Mbinu bora za kulima na kwa wakati ufao. • Mfumo wa kupanda mimea kwa mzunguko.
• Mbolea ya kijani na vibweta-kunde.
• Boji-ezefu kufunika mchanga ulio wazi.
Kukabili wadudu na kwekwe:
• Uangalifu katika kuchagua aina ya mimea
• Matumizi ya mimea iliyo na uwezo wa kuhimili ukame au janga la wadudu
na magonjwa.
• Mbinu bora za kulima na kutayarisha shamba.
• Mzunguko wa mimea au kupanda kwa zamu.
• Kuendeleza mahasimu wanaoangamiza wadudu.
• Kuimarisha nasaba ya kizazi.
• Matumizi ya dawa za kiasili kukabili wadudu.
Kadhalika Kilimo hai hujumuisha:
• Matumizi bora ya maji.
• Ufugaji bora.
| Attachment | Size |
|---|---|
| swahili notes kilimohai.pdf | 482.58 KB |
| madawa asili.pdf | 185.73 KB |
| KANUNI ZA KILIMOHAI .pdf | 1.48 MB |
